Brazil imekuwa taifa la kwanza kufuzu
kwa fainali za Kombe la Dunia ambazo zitachezewa nchini Urusi mwakani. Timu
hiyo ilifuzu baada ya
kulaza Paraguay 3-0, nao Argentina na Uruguay wakashindwa.
Brazil waliwashinda Paraguay kupitia mabao ya mshambuliaji wa
Liverpool Philippe Coutinho, nyota wa Barcelona Neymar ambaye pia alipoteza
mkwaju wa penalti na mchezaji wa Real Madrid Marcelo.
Brazil kwa sasa wamo alama tisa mbele ya Colombia ambao
wanashikilia nafasi ya pili. Huo ulikuwa ushindi wa nane kwa Brazil chini ya
Tite.
Paraguay, wamo alama chini ya nne bora, zikiwa zimesalia mechi
nne kuchezwa.
Argentina wanakabiliwa na kibarua kufuzu baada ya kushindwa 2-0
na Bolivia na kushuka hadi nambari tano, alama moja nyuma ya Chile.
Uruguay, waliochapwa 2-1 na Peru mjini Lima Jumanne, wamo
nambari tatu.
Taifa litakalomaliza nafasi ya tano litacheza mechi mbili za
muondoano (nyumbani na ugenini) dhidi ya taifa kutoka Oceania.
0 comments:
Post a Comment