Vikosi vinavyoshughulikia doria za baharini katika bandari ya
Hodeidah inayodhibitiwa na waasi Wa-houthi vinasema boti hiyo ilikuwa inatoka
Yemen kuelekea Sudan wakati liliposhambuliwa kwa kombora.
Kituo cha habari kinachomilikiwa
na waasi hao kimedai shambulio hilo limefanywa na ndege ya hlikopta aina ya
Apache ambapo zaidi ya majeruhi 80 wa mkasa huo wamekimbizwa hosptialini.
Eneo la Hodeidah ni mojawapo linalokumbwa na mashambulio ya mara
kwa mara kutokana na mzozo wa kivita unaoendelea baina ya jeshi la Yemen
linaloungwa mkono na lile la Saudia, dhidi ya waasi hao wa Houthi wanaopinga
serikali ya Yemen.
0 comments:
Post a Comment