PROF. MBARAWA AKAGUA JENGO LA WIZARA YAKE MJINI DODOMA

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ametembelea ujenzi wa jingo litakalokuwa na ofisi za wizara hiyo mjini Dodoma, hii ni katika kutekeleza agizo la Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuhamia makao makuu ya nchi mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (Sekta ya Ujenzi) Dkt. William Nshama wakati alipokagua maendeleo ya Jengo jipya la Ofisi za Wizara hiyo lililoko Mtaa wa Moshi, mkoani Dodoma.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (Sekta ya Ujenzi) Dkt. William Nshama wakati alipokagua maendeleo yaliyofikiwa ya mgawanyo wa ofisi katika Jengo jipya la Wizara hiyo lililoko Mtaa wa Moshi, mkoani Dodoma.

Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (Sekta ya Ujenzi) Dkt. William Nshama akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu hatua zilizofikiwa katika Jengo jipya la Ofisi za Wizara hiyo lililoko Mtaa wa Moshi, mkoani Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (Sekta ya Ujenzi) Dkt. William Nshama (katikati), wakati alipokagua na kuona mgawanyo wa Ofisi kwa Sekta zake katika Jengo jipya la Wizara hiyo lililoko Mtaa wa Moshi mkoani Dodoma. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Eng. Ven Ndyamukama.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment