Fifa
imetangaza kuifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai ya
serikali kuingilia masuala ya soka.
Waziri wa Michezo wa
Mali, Housseini Amion Guindo aliamua kuunda kamati ya muda kuendesha Shirikisho
la Soka la Mali (Femafoot) baada ya kuona uongozi uliokuwa madarakani kutokuwa
sahihi.
Lakini
baada ya Femafoot kufikisha malalamiko yake FIFA, shirikisho hilo la soka la
limataifa, likaiamuru serikali ya Mali, kuvunja kamati hiyo hadi Ijumaa.
Baada ya kuona hakukuwa na utekelezaji hadi leo usiku huku zikiwa zimebaki saw chache kabla ya muda kufika, Fifa imetangaza kuifungia Mali.
Baru iliyoandikiwa nchi ya Mali kutoka FIFA |
0 comments:
Post a Comment