Joseph Lamptey |
Refa ambaye ni raia wa Ghana Joseph Lamptey, amefungiwa maisha kutochezesha mechi ya aina yoyote na shirikisho la kandanda Duniani Fifa, baada ya masuali kuibuka jinsi alivyosimamia mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia kati ya Senegal na Afrika Kusini Novemba 2016, iliyopita.
Afrika Kusini ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1 lakini Senegal
ikalalamika kwa shirikisho la Fifa, Walisema kuwa Lamptey aliwapa Afrika kusini
penalti licha ya naibu refa kuashiria kuwa ingekuwa kona.
Wengi waliuliza maswali kuhusu kona hiyo wakati huo, kikiwemo
kitengo cha michezo cha BBC kilichoripoti kuwa Afrika Kusini iliongoza baada ya
panelti hiyo yenye utata
0 comments:
Post a Comment