Umoja wa Madaktari,
Wauguzi na Wataalamu wa Meno nchini Kenya ‘Kenya Medical Practitioners,
Pharmacists and Dentists’ Union’ (KMPDU) umepinga vikali hatua ya Serikali ya
Kenya kuleta madaktari kutoka Tanzania wakati Kenya ina madaktari wengi ambao
hawaajiriwa.
Kupitia kwa Katibu Mkuu
wa KMPDU, Ouma Oluga umepinga hatua hiyo na kudai kuwa Serikali ya Kenya
haijawa makini katika kushughulika na tatizo la upungufu wa madaktari nchini
humo.
Akizungumza na mtandao wa The Star wa nchini
Kenya siku ya Jumamosi, Oluga alisema hata hivyo watawakaribisha madaktari
kutoka Tanzania na kuwaunganisha katika umoja huo na kwamba watapaswa kupitia
mitihani itakayoandaliwa na bodi ya wauguzi.
Amesema mitihani hiyo
itachukua sio chini ya miezi mitatu labda kama tu hitaji hilo halitaangaliwa.
“Kenya ina zaidi ya
madaktari 1,400 ambao wanasubiria ajira. Itakuwa gharama kubwa na dalili ya
kushindwa kutumia fedha za umma vizuri kwa kuwa na madaktari 500 wa kitanzania
kwa gharama ya Shilingi 20,000 kwa siku,” amesema.
Oluga amesema kuwa Kenya
inapaswa kupitia upya utaratibu wake wa Rasilimali Watu kwa mujibu wa miongozo
ya Afya kama ambavyo KMPDU imekuwa ikihitaji hapo kabla. “Hatuwezi kuwa
tunafanyia majaribio maisha ya wakenya katika hali inayoonesha kutowajali
wananchi,” ameongeza.
Mapema jana Rais Magufuli
alikubali na kuridhia ombi la Serikali ya Kenya na kuahidi kutuma madaktari 500
kusaidia kukabiliana na tatizo la upungufu wa madaktari nchini humo kufuatia
mgomo wa madaktari ulioisha hivi karibuni baada ya kudumu kwa siku 100.
0 comments:
Post a Comment