ZANZIBAR KULIPA DENI TANESCO


Waziri wa Nishati, Prof. Muhongo amewatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa hawatakatiwa umeme baada ya SMZ kuanza kulipa deni inalodaiwa ni baada ya siku chache tangu itangazwe kwamba Zanzibar itazimiwa umeme endapo haitalipa deni hilo.  
Tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kulipa deni la shilingi bilioni 10 linalodaiwa na shirika la umeme Tanzania TANESCO, na itaendele kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika.
“Tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imeanza kulipa kiasi cha Shilingi bilioni 10 na itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika” alisema Prof. Muhongo.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment