Mke wa aliyekuwa mchezaji wa Ghana
Michael Essien ameinunua klabu ya ligi ya tatu Como ,kulingana na klabu hiyo. Akosua Puni Essien ameripotiwa kulipa pauni
206,000 katika mnada wa klabu hiyo iliofilisika.
Mmiliki mpya na timu yake sasa ana mpango wa kuimarisha kikosi
cha kwanza pamoja na ile timu ya vijana kukuwa. Wataweka juhudi za kuifanya
kurudi katika Serie B na kukuza vipaji vya vijana waliomo.
Puni Essien amejielezea kuwa mfanyibiashara ,mshauri, mtu
anayependa kusaidia na mama wa watoto watatu.
Como imeshiriki mara kadhaa katika ligi ya daraja la kwanza ya
Seria A ,ikiwa imecheza sana kati ya 1984 hadi 1989 na hivi majuzi ikiwa
2002-2003 ambapo walishushwa daraja baada ya msimu mmoja.
0 comments:
Post a Comment