MSEMAJI WA JESHI LA POLISI UGANDA AUAWA

Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.
Taarifa zinasema Bw Kaweesi na walinzi wake wawili walioandamana nae wameuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa akika nyumbani kwake Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.
Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.
Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.

Aliyekuwa msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda


Gari ambayo alikuwa amepanda Felix Kaweesi na walinzi wake wawiili
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment