Waziri wa katiba na sharia Dkt.
Harson Mwakyembe amepiga marufuku watu kufunga ndoa aina yeyote, ya kiserikali,
kimila ama kidini bila ya kuwepo vyeti vya kuzaliwa vya wanafunga ndoa.
Waziri huyo ameyasmea hapo
alipokuwa katika ziara yake mkoani Morogoro na kuogeza kwamba serikali imeamua
hivyo ili kupata takwimu za wananchi wake zitakazowawezesha kupanga mipango ya
maendeleo sambamba na kuzuia uhamiaji haramu.
Pia amewataka wakala wa
usaili wa vizazi na vifo (RITA) kuhakikisha inasimamia sharia ya usajili na
kusema kwamba endapo hakutakuwa na takwimu sahihi za vizazi na vifo ama ndoa
inasababisha nchi kutosonga mbele kimaendeleo.
“Wenzetu nchi zilizoendelea
suala la usaili wamelipa kipaumbele lakini sisi bado tuko nyuma, mfano mkoa wa
Morogoro kwa mujibuwa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonesha jumla ya
wakazi milioni 2.2 lakini waliosailiwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni 11%
pekee, huku wengine wakiwa bado” alisema Mwakyembe
Agizo hilo litaanza kutimizwa mwei Mei mosi mwaka huu
0 comments:
Post a Comment