Shirika
la Afya Duniani limesema watoto milioni 116 watapa chanjo ya ugonjwa wa kupooza
wa polio katika nchi 13 za Afrika magharibi na Afrika ya Kati kama sehemu ya
jitihada za kuangamiza maradhi hayo barani Afrika.
Mpango
huo utawalenga watoto wote wa chini ya miaka mitano katika nchi hizo 13 ikiwamo
Benin, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Côte d'Ivoire, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Guinea, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Nigeria na
Sierra Leone.
Mkurugenzi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF kwa nchi za Afrika
magharibi na Afrika ya Kati Marie-Pierre Poirier amesema ana matumaini kuwa
ugonjwa wa polio utatokomewzwa barani humo kwa msaada wa viongozi wa Kiafrika
0 comments:
Post a Comment