Shirika la
umeme Tanzania (Tanesco), linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 4 na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) za kodi ya mitambo ya kuzalisha umeme iliyokwama katika
Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Akizungumza na wanahabari Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Nishati na Madini, Deo Ngalawa, baada ya kutembelea mradi wa
uzalishaji wa umeme wa gesi asilia wa Kinyerezi, Dar es Salaam, alisema kuwa
mitambo hiyo iliingizwa nchini ili kuongeza uzalishaji wa umeme.
“Tanesco inadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 4 na TRA, deni hilo
linatokana na kukwama kwa mizigo ya kuzalisha umeme, ikiwamo mitambo na
jenereta kutoka nje ya nchi, jambo ambalo linachangia kurudisha nyuma
uzalishaji wa umeme,” alisema Ngalawa.
Aidha alisema maeneo mengi ya mradi huo yanahitaji kuwekwa mitambo
ambayo imezuiliwa kutoka kutokana na deni hilo, hivyo watazungumza na serikali
kuona namna ya kutatua changamoto hiyo.
0 comments:
Post a Comment