Wanamuziki machachari wa
muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz na Ally
Kiba wamekataa kuimba kolabo ambayo ilitarajiwa kuwa ndio wimbo wa hamasa kwa
ajili ya kuhamasisha vijana wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17
Serengeti Boys katika michuano ya vijana Afrika nchini Gabon.
Taarifa hyo imetolewa na
Maulid Kitenge katika ukurasa wake wa Twitter, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya uhamasishaji ya
Serengeti Boy, amesema “Kiba na Diamond wameshindwa kuonesha uzalendo kwa
Serengeti Boys wamegoma kuimba wimbo wa hamasa licha ya kuwepo kamati ya hamasa,
inasikitisha”
Wasanii hao ambao pia ni
wajumbe wa kamati ya uhamasishaji ya Serengeti Boys wamefikia uamuzi huo huku
wengi wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya na wapenzi wa mpira wa miguu
wakitegemea kolabo ya wasanii hao katika wimbo wa kuhamasisha Srengeti Boys. Wasanii hao walitegemewa kuingiza kuimba kolabo hiyo na
wasanii wengine ambao ni Darasa, Mwasiti Almas, na Vanesa Mdee
0 comments:
Post a Comment