Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kesho tarehe 28 April 2017 atapokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa Umma katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
Taarifa hiyo itawasilishwa kwa Mhe. Rais Magufuli na
waziri wa nchi ofisi ya rais na menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora
mheshimiwa Angela Kairuki ambapo zoezi hilo limechukua takribani miezi sita
sasa tangu mwezi Oktoba mwaka 2016
0 comments:
Post a Comment