Madaktari waliotakiwa kwenda
kuhudumu nchini Kenya kulikokuwa na uhaba wa madaktari kutokana na mgomo wa
madaktari nchini humo wameitwa kazini rasmi na wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Tangazo hilo limekuja mara
moja kufuatia agizo la Rais la kuwapatia kazi madaktari hao walioonesha nia ya
kwenda kufanya kazi nchini Kenya.
Tangazo hilo limetolewa na
katibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na
kuwataka madaktari hao kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi siku kumi nan ne (14)
kuanzia siku ya tangazo hili. Waliopamgiwa TAMISEMI wametakiwa kuripoti Ofisi
za TAMISEMI Ddodoma na waliopangiwa wizarani warripoti Ofisi ndogo za Wizara
Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment