.
Jumuiya
ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unatoa pongezi kwa Wabunge wa Bunge Tukufu
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia,
kikatiba na kikanuni kufanikisha uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki
uliofanyika tarehe 4/4/2017 bungeni mjini Dodoma.
Pia
unawapongeza Wabunge waliochaguliwa kuiwakilisha nchi yetu katika Bunge la
Afrika Mashariki, tunawataka kuwa wazalendo,
waadilifu, wachapakazi na wenye kutanguliza maslahi ya nchi yetu Tanzania.
Pia, UWT imeridhishwa na hatua za mchakato
wa uchaguzi huo ndani ya Bunge na inapongeza demokrasia pana, komavu na
shirikishi iliyooneshwa na wabunge kwa kupiga kura ya HAPANA kwa wagombea
waliotokana na CHADEMA kwa sababu uteuzi wao haukuzingatia misingi ya
demokrasia, uwakilishi wa Kitaifa wala jinsia.
Uteuzi uliofanywa na CHADEMA
hata baada ya kushauriwa, unadhihirisha dharau kubwa na kutothamini mchango wa
Wanawake wa Tanzania katika maendeleo ya nchi yetu.
Bunge na Wabunge lazima wawe
mstari wa mbele katika juhudi za kuimarisha demokrasia yetu kama Taifa na ndani
ya vyama vya siasa, kamwe Bunge lisiruhusu kutumika kama “rubber stamp” kama
ambavyo CHADEMA walipanga kwa kuteua wagombea wawili pekee na kwa kufanya hivyo
tayari waliamua nani awe mbunge na kulinyima Bunge fursa na uhuru wa kuchagua
miongoni mwa wagombea.
Aidha, UWT imesikitishwa sana
na kauli za MATUSI, DHARAU na KEJELI alizozitoa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani
Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe dhidi ya Wabunge na Bunge
Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kitendo cha Mhe. Mbowe
kuwatukana Wabunge sio tu kinakiuka Kanuni za Maadili ya Viongozi lakini pia
kinatweza UTU na HESHIMA ya wabunge na bunge mbele ya jamii.
UWT inaungana na Maamuzi ya
Mhe. Spika ya Kuwaita watovu wa nidhamu kwenye Kamati ya Maadili.Hata hivyo
tunamtaka Mhe. Freeman Mbowe kuomba radhi wabunge na Umma wa Tanzania kwa lugha
isiyo na staha.
Pamoja na kuomba radhi,
tunamtaka Mhe Mbowe afute kauli yake ya kuwahusisha na kuwatuhumu Viongozi wa
Serikali (Rais na Waziri Mkuu) na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuwa
wameingilia uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ndani ya Bunge.
UWT inaendelea kuwahimiza
Wabunge kujadili na kupitisha Bajeti kwa kuzingatia vipaumbele muhimu kwa
Maendeleo ya Jamii na Ukuaji wa Uchumi ikiwemo Ujenzi wa Miundombinu ya Maji,
Afya, Elimu, Umeme Vijijini, pamoja na kuimarisha njia za Uchukuzi na
Mawasiliano k.v Barabara na Reli.
0 comments:
Post a Comment